Kupata mwema rafiki,sala yapasa shiriki,
Wako wengi wanafiki,tena vinara wa chuki,
Jaribu kumhakiki,Mola akupe a haki,
Rafiki
hutomjua,asilani abadani.
Rafiki mfano nyuki,utaishia mikuki,
Atakujaliza dhiki,na kukujaza mikiki,
Hutoipata riziki,kwa rafiki alo “shirki”,
Rafiki
hutomjua,asilani abadani.
Wengi wao wazandiki,shida hawatoshiriki,
Misibani hawatoki,kukung’ong’a watabaki,
Utabaki kuhamaki,furaha hutomiliki,
Rafiki
hutomjua,asilani abadani
Konisaga Mwafongo-0717
248828/0767 24 88 28 Mbeya.
No comments:
Post a Comment