umezidi kuongopa,watu tunakuogopa,
uongo unaotupa,ni shetani amekupa,
kwa Mungu ungejitupa,ni baraka angekupa,
uongo ulionao,wote tunakuogopa.
ulisema kaka yako,ni msaidizi wako,
kumbe halikuwa kwako,bali ni kinywani mwako,
kumfanya mbwa koko,au ya embe makoko,
uongo ulionao,wote tunakuogopa.
ulisemalo kinywani,kumbe hunalo moyoni,
watufanya hayawani,kama kitanda chumbani,
kutoka mkutanoni,waeleza vilabuni,
uongo ulionao,wote tunakuogopa.
janga litapokukumba,tamlilia muumba,
sasa mali unatimba,umesahau kuomba,
wafanya hata vilemba,umekuwa sawa mamba,
uongo ulionao,wote tunakuogopa.
No comments:
Post a Comment