Thursday, September 8, 2011

SHIDA HAINA ADABU.

kila mtu ana shida,ingawa hazifanani,
shida haijali muda,wala una kazi gani,
shida ni sawa husuda,hivi leo ninaghani,
  shida haina adabu,jamani nawaeleza.

shida inapokupata,sana unahangaika,
pumzi utaivuta,na jasho litakutoka,
majonzi yatafuata,mwili ukatetemeka,
  Jahazi laenda kombo,naogopa tutazama.

shida inapokupata.waweza omba mkopo,
upunguze furukuta,mfano ule wa popo,
lipa deni kulifuta,ulikopa kwa kiapo,
  Jahazi laenda kombo,naogopa tutazama.

wengi tunawashangaa,shida inapowapata,
waja kwa kunyenyekea,tena mwendo wa kunyata,
shida wakielezea,huruma inakupata,
  Jahazi laenda kombo,naogopa tutazama.

nisemayo ni hakika,jaribu kujiuliza,
kama halijakufika,sasa ninakueleza,
 akilini lifutika,wasije wakakuliza,
  Jahazi laenda kombo,naogopa tutazama.

ahadi kweli ni deni,ukikopa kweli lipa,
usiufanye uhuni,kwa imani alikupa
sasa vipi wamuhini,hutaki deni kulipa,
  Jahazi laenda kombo,naogopa tutazama.

No comments:

Post a Comment