udereva kazi ngumu,sana ukifikiria,
kuendesha ni vigumu,sukani kushikilia,
umakini ni muhimu,ajali sije tokea,
Endesha gari vizuri,ajali kuziepuka.
gari unaliendesha,kwa raha mustarehe,
njiani unatushusha,hata kwenye masherehe,
safari kweli yachosha,pamoja ni starehe,
Endesha gari vizuri,ajali kuziepuka.
gari hili tuthamini,kila mtu alipenda,
unapofika kitini,ni wasaa kulipenda,
mafuta simwage chini,ni sawa pesa kuponda,
Endesha gari vizuri,ajali kuziepuka.
kiti ni cha kukalia,sio kusimama juu,
matope watupakia,hatuyapendi makuu,
sasa hivi umekua,wewe sio mjukuu,
Endesha gari vizuri,ajali kuziepuka.
gia nikanyage vipi,mafuta yamezagaa,
miguu niweke wapi,nimebaki nashangaa,
hili gari ni kwa vipi,mafuta yatapakaa,
Endesha gari vizuri,ajali kuziepuka.
No comments:
Post a Comment