Wednesday, September 14, 2011

TUELEZANE UKWELI

utnzi ni kazi ngumu,japo tunaitamani,
kupanga beti vigumu,tena ziwe na thamani,
upatapo jambo gumu,lisumbue akilini,
  Tuelezane ukweli kama kweli twapendana.

nikuonapo yakini,moyo wangu hupasuka,
binti uliye makini,tena ulivyoumbika,
mimi nitafanya nini,kutwa ninaweweseka,
  Tuelezane ukweli kama kweli twapendana.

mara nyingi nimewaza,nikwambie kitu gani,
huenda utapuuza,kuniona hayawani,
jibu safi lanipoza,kama maji mtungini,
Tuelezane ukweli kama kweli twapendana.

mengi ya kusema sina,ushairi siujui,
naomba jibu mwanana,jeupe mfano tui,
usinione wa jana,au ni mtu sifai,
Tuelezane ukweli kama kweli twapendana.

No comments:

Post a Comment