Sunday, September 18, 2011

KWA NINI?

mimi nawaza kwa nini,inatokea kwa nini,
mkono kuwa shavuni,nikiwapo mawazoni,
mbona siweki begani,au kuweka shingoni,
  Nini kinasababisha,mkono kuwa shavuni?

hata kwenye mitihani,wewe jaribu chunguza,
akili zipo kichwani,sana muda utawaza,
mkono upo shavuni,kichwani kupeleleza,
  Nini kinasababisha,mkono kuwa shavuni?

habari ya kushtusha,mikono kuwa kichwani,
 kwa nini hukuishusha,kuipeleka shavuni,
sasa nini chakuchosha,jijadili akilini,
  Nini kinasababisha,mkono kuwa shavuni?
jambo linalokutisha,waiweka na kutoa,
 lile la kusikitisha,shavuni wajiwekea,
 mawazo yakikutosha,waenda kujilalia
  Nini kinasababisha,mkono kuwa shavuni?

No comments:

Post a Comment