Monday, September 19, 2011

MWALIMU

kila mtu ni mwalimu,tofauti taaluma,
wapo wa mambo muhimu,na wengine maamuma,
wapi tapata rasimu,sipendi jiumauma,
  kila mtu ni mwalimu,wengi si kitaaluma,

akufundishaye jambo,huyo kwako ni mwalimu,
hata kama kwa vikumbo,sheria utasalimu,
wataka kujua mambo,hutoogopa hukumu,
kila mtu ni mwalimu,wengi si kitaaluma,

baba aliyekuzaa,huyo ni mwalimu wako,
 mama aliyekulea,naye ni mwalimu wako,
 jirani penye mtaa,ajua tabia zako,
kila mtu ni mwalimu,wengi si kitaaluma,
yule babako mzazi,yeye ni mwalimu wako,
 akifanya ubazazi,hiyo ni elimu yako,

 kama yeye mchochezi,huo ni urithi wako,

kila mtu ni mwalimu,wengi si kitaaluma,


mama mpika majungu,hiyo ni elimu yako,
 wamsuta kwa uchungu,kwake yeye ni karamu,
 enda chini ya uvungu,ni wapi mwana adamu,
kila mtu ni mwalimu,wengi si kitaaluma,


baba kutwa amenuna,anawapa somo gani,
 hakuna raha hakuna,watu wote ni huzuni,
 watoto wakikuona,hujificha uvunguni,
kila mtu ni mwalimu,wengi si kitaaluma,

No comments:

Post a Comment