Wednesday, September 21, 2011

HONGERA NYASA HONGERA

gazeti nyasa hongera,nyanda za juu kusini,
mambo yaliyotukera sasa,wazi gazetini,
sasa simama imara,upafike kileleni
hongera nyasa hongera,umeleta ukombozi

zamani tilipunjika,mwanya finyu tulipewa,
mambo mengi kufichika,wengi hatukuelewa,
sasa yaanza fichuka,mengi yatakuwa sawa,
hongera nyasa hongera,umeleta ukombozi

kupata gazeti letu,hakika,tunashukuru,
 tutaona mambo yetu,kweli huu ni uhuru,
 hata vijijini mwetu,tumeshapata uhuru,
hongera nyasa hongera,umeleta ukombozi

makala za kuvutia,'kama ninasema hivi'
 zote mnatupatia,hakika ninyi wajuvi,
 mashairi yavutia,kama mahiri wavuvi,
hongera nyasa hongera,umeleta ukombozi

habari za vijijini,sasa tunajipatia,
 tulihamia mijini,riziki jitafutia,
 sasa tunayabaini,maendeleo sawia.
hongera nyasa hongera,umeleta ukombozi

 limeshafika Mshewe,kwake mzee Mwangoka,
 liliwatia kiwewe,moyoni kufarijika,
 hebu jiulize wewe,mangapi ulipunjika,
hongera nyasa hongera,umeleta ukombozi

kaulize Ibungila,kama hawajaliona,
 hata ufike Lumbila na majirani Kagwina,
 kwake kaka mwasubila,nyasa kwake ajivuna,
hongera nyasa hongera,umeleta ukombozi

limefika hata Mbozi,kwake Richadi Ayao,
 ameweza nipa dozi,ushauri wa kikwao,
 nami natoa pongezi,nyasa limefika kwao,
hongera nyasa hongera,umeleta ukombozi

hongereni,waandishi,pia nanyi wahariri,
 kujifunza na kuishi,kzai yenu ni mahiri,
 msiandike uzushi mtapata soko zuri,
hongera nyasa hongera,umeleta ukombozi

No comments:

Post a Comment