Monday, September 19, 2011

TURUDI KWETU

watu wetu watu wetu,sasa na turudi kwetu,
huko sasa sio kwetu,turudi na vitu vyetu,
sipapendi huko katu,twapoteza mila zetu,
  sasa na turudi kwetu,tujivunie vya kwetu.

nimeona vitu vingi,sisemi uongo katu,
pia nimeona watu,akili zao ni fyatu,
hila mfano wa chatu,au sawa mbwa mwitu,
  Jamani tutafakari,tupate ndoa imara.

utamaduni si wetu,tujivunie vya kwetu,
 vimini si jadi yetu,suruali sio zetu,
 pedo sitavaa katu,kwani mimi si kifutu,
  Jamani tutafakari,tupate ndoa imara.

sasa sisi tuwe watu,tuenzi taifa letu,
 kuiga mila za watu,twaua vizazi vyetu,
 mila si sawa viatu,kuvaa vya kila mtu
   Jamani tutafakari,tupate ndoa imara.

No comments:

Post a Comment