ndoa ni kitu kizuri,sana ukitafakari,
nyingi kama utiriri,nyingi sana zina heri,
hebu jaribu fikiri,uone wake uzuri,
Jamani tutafakari,tupate ndoa imara.
mambo mengi yanajiri,hebu tuache kiburi,
ndoa si sawa futari,inataka umahiri,
ndoa sio kukariri,ndani ya madaftari,
Jamani tutafakari,tupate ndoa imara.
ndoa hakika safari,inataka wenye heri,
ukijitia kafiri,utaiona saburi,
yapasa uwe mahiri,kushinda hiyo safari
Jamani tutafakari,tupate ndoa imara.
ndoa ni kitu kizuri,hupaswi kuwa na mori,
usiwe nayo jeuri,kama vile paka pori,
ukijitia mpori,tengano lawasubiri,
Jamani tutafakari,tupate ndoa imara.
No comments:
Post a Comment