Tuesday, September 20, 2011

HONGERA WAHITIMU

naanza kuwasalimu,ninyi mnaohitimu,
sasa nashika kalamu,kuwapa yale muhimu,
kujali muda muhimu,sote tunaohitimu,
Ingawa mnahitimu,kuwa nanyi twatamani.

mtawaacha walimu,pindi mkijaza fomu,
yawapasa mfahamu,maisha huko magumu,
Mola ndiye ufahamu,hilo budi mfahamu,
Ingawa mnahitimu,kuwa nanyi twatamani.

mmekuwa kama timu,kushinda wote ugumu,
 vipindi zamu kwa zamu,waliwafunza walimu,
 ili mpate fahamu,mlipokea kwa hamu,
Ingawa mnahitimu,kuwa nanyi twatamani.

Mola mnamfahamu,wa baba yetu Adamu,
 Mungu mkamuheshimu,kimafunzo mmedumu,
 nanyi ni wana adamu,kutii dumu dawamu,
Ingawa mnahitimu,kuwa nanyi twatamani.

 hakika mmefahamu,elimu ni ya muhimu,
 mtakuwa watalamu,umma kuupa fahamu,
 yale mlopata humu,jalini ubinadamu
Ingawa mnahitimu,kuwa nanyi twatamani.

No comments:

Post a Comment