wazazi tulionao,ni mola katujalia,
hata kama haunao,Muumba kawachukua,
aliwapa na uzao,watoto kawapatia.
wazazi tulionao,halahala tuwatunze.
mola kawapa ukoo,unaoweza kukua,
si kama ule wa koo,watoto kutowalea,
watoto sio popoo,yapasa kuangalia,
wazazi tulionao,halahala tuwatunze.
tusikabane makoo,pesa ili watumia,
sana twalizua soo,usoweza fikiria,
wao si kidali poo,kuweza kuwachezea,
wazazi tulionao,halahala tuwatunze.
hebu tazama kioo,ndiko walikotokea,
hauhitaji apio,ujana walipitia,
wewe sawa na minyoo,wazazi kuwachukia,
wazazi tulionao,halahala tuwatunze.
wao wakisema ndio,baraka utapokea,
baraka watoa wao,mambo yatunyookea,
wao sawa na kinoo,njia kutusafishia,
wazazi tulionao,halahala tuwatunze.
No comments:
Post a Comment