tabia mbaya ni nyingi,ni sawa wingi wa watu,
nitayaongea mengi,aibu sioni katu,
nimeona watu wengi,roho zimejaa kutu,
tuache tabia mbaya,duniani tupendane.
mara nyingi nimeona,mambo ya kusikitisha,
matajiri wajiona,sana inaogopesha,
fukara wakituona,magari tope yarusha
Jahazi laenda kombo,naogopa tutazama.
wafika nyumbani kwangu,kuja kunitembelea,
nakuona ndugu yangu,upendo twajijengea,
ninapokaa si pangu,mimi nimejipangia
Jahazi laenda kombo,naogopa tutazama.
umekaa sebuleni,macho macho yako pekupeku,
wachungulia chumbani,nini uliacha huku,
si vizuri asilani,wewe sio panya buku,
Jahazi laenda kombo,naogopa tutazama.
mezani kuna barua,nimeandikiwa mimi,
bado sijaifungua,imetoka kwa Msami,
wewe unaichukua,unajitia msomi,
Jahazi laenda kombo,naogopa tutazama.
jambo hili la barua,sana linanichukiza,
leo hii naamua,nilitoe kwenye giza,
kama umeifungua,uijibu nakweleza,
Jahazi laenda kombo,naogopa tutazama.
No comments:
Post a Comment