Sunday, September 18, 2011

ULIDHANI UNAJUA

hakika wajidanganya,ukidhani ni mwenzako,
urafiki mlifanya tena kwa mafanikio,
akili hukuikanya,tena kwa mfatilio,
  Ulidhani unajua,kumbe unajidanganya.


shule mlisoma wote,na tena darasa moja,
mliongozana kote,tena kwa ule umoja,
mpira kucheza wote,mlikuwa halimoja,
Ulidhani unajua,kumbe unajidanganya.

mtaa wenu mmoja,tena kuitana ndugu,
 sisi mnazi mmoja,na wao kwao ni Pugu,
jambo tulilolingoja sasa imekuwa pwagu
Ulidhani unajua,kumbe unajidanganya.
wakumbuke marafiki,mlipokuwa watoto

No comments:

Post a Comment