Tafsiri nimejua,mtu jibu kutotoa,
sana anafikiria,vipi atakupatia,
pengine anadhania,ni vigumu kuongea,
Kila akaaye kimya,jibu lake ni mwanana.
Si lazima akwambie,ndipo ulipate jibu,
wala umsogelee,awe japo kwa karibu,
au sana muongee,ajifunue hijabu,
Kila akaaye kimya,jibu lake ni mwanana.
No comments:
Post a Comment