mtoto akizaliwa,lazima apewe jina,
kupata ni majaliwa,kulazimisha hapana,
hakika nimeelewa,kwa marefu na mapana,
Tumieni jina langu,na sio mama fulani
mara nyingi nimeona,matumizi ya majina,
mengi yanavyofanana,na tena yanagongana,.
watu wanapoitana,majina yao mwanana,
Tumieni jina langu,na sio mama fulani
mimi ninaye mtoto,jina aitwa aleni,
sijampata kwa ndoto,kanipatia manani,
haikuwa wangu wito,sasa ninaye nyumbani,
Tumieni jina langu,na sio mama fulani
akijalia manani,wazazi zawadi kuu,
jina lako ni jamali,katu sipende makuu,
mtoto wako ni Ali,wewe baba ya Abuu,
Tumieni jina langu,na sio mama fulani
unabagua watoto,kutumia jina moja,
wewe ni mama Kizito,mumeo baba Mhoja,
wajiita mama wini,sisi watupa utata,
Tumieni jina langu,na sio mama fulani
watoto kuwabagua,ni dhambi kubwa kwa Mola,
jina moja wachagua,ndugu yangu Halahala,
baba John nakwambia,kamwambie na Hamala,
Tumieni jina langu,na sio mama fulani
No comments:
Post a Comment