kuna jambo lakutinga,nakuomba niambie,
lipo jambo ulipanga,bora nifafanulie,
ni mawazo yakusonga,si' tukufafanulie,
kaza moyo niambie,ni lipi linakutinga.
twaishi sote chumbani,mimi nikiwa mkeo,
usilete tafrani,ninalueleza leo,
sura yako taabani,mikunjo bila mkao,
juzi uliniambia,wataka mke wa pili,
mimi niliridhia,tamaa zako za mwili,
macho leo nikazia,tena ni mwezi kamili,
Ulidhani unajua,kumbe unajidanganya.
uchumba tulipoanza,wala hukuleta manza,
ni wewe ulinianza,kunitoa kwetu Mwanza,
imani imeniponza,tangu uchumba kuaanza,
Kaza moyo niambie,ni lipi linakusibu
kutwa kucha umenuna,nyumbani hapakaliki,
wiki tatu nimeona,jikoni hapapikiki,
siwezi hata jikuna,sebule haikalilki,
. Kaza moyo niambie,ni lipi linakusibu
kwetu jiko haliwaki,wewe unakula wapi,
uyafanyayo si haki,hata kama ni kwa 'popi;,
wewe wala mishikaki,mimi ni maji na pipi,
Kaza moyo niambie,ni lipi linakusibundoa kitu cha hiyari,sio kulazimishana,
kaa vizuri fikiri,tusije ngeo toana,
moyoni nilitabiri,siku tutafarakana,
Kaza moyo niambie,ni lipi linakusibu
umeshindwa kunambia,mimi nasema nakwenda,
sipendi kuambulia,kwa wenzio kuniponda,
Mungu atanijalia,raha nami nitaponda
Kaza moyo niambie,ni lipi linakusibu.
No comments:
Post a Comment