Sunday, September 18, 2011

CHAMA

chama hiki chama chetu,sote tunalitambua,
chama kinajali utu,sote tunakiimbia,
sio chama cha upatu,pesa kikatuibia,
  chama kikishakuchoka,hakika utagundua.

mialiko ya kichama,katu hutoisikia,
ulizoea 'minyama',hata supu ya mkia,
kujirusha na 'mimama',hata na vichangudoa,
  chama kikishakuchoka,hakika utagundua.

shangingi hutolipanda,miguu yako ni gari,
 mwanga ulioupenda,wako sasa kibatari,
 hivi sasa wakuponda,kama ya jana futari,
  chama kikishakuchoka,hakika utagundua.

No comments:

Post a Comment